Chanjo za COVID-19 na wagonjwa wa Kifafa

Image of flag of Kenya used to denote Swahili

Chanjo dhidi ya COVID19 sasa zinapatikana. Tunapendekeza kwamba watu walio na kifafa wanapaswa kupokea chanjo ya COVID19 inapopatikana; hii ni pamoja na dozi ya nyongeza. Kwa watu wenye kifafa, hatari ya kuambukizwa COVID-19 na kuzuka kwa madhara zaidi ya kiafya, inapita athari hasi za chanjo ya COVID-19.

Kwa sasa hakuna ushahidi unaoashiria kama, kuwa na ugonjwa wa kifafa kunachangia kuibuka kwa athari hasi kutokana na chanjo ya COVID-19, hasa kuongezeka kwa mshtuko. Lakini, kama ilivyo na chanjo zingine, homa inaweza kuzuka baada ya kupokea chanjo ya COVID-19. Hii inaweza kuongeza matukio ya kuanguka kwa baadhi ya wagonjwa wa kifafa. Lakini, wakitumia madawa ya homa, kama vile Paracetamol /acetaminophen kwa muda wa masaa 48 baada ya chanjo aukipindi chote wanachougua homa, hatari hii inapungua.

Kabla ya kupokea chanjo ya COVID-19, hakikisha umemjulisha anayetoa huduma ya chanjo kuwa wewe ni mgonjwa wa kifafa. Kadhalika mpe taarifa zingine muhimu kuhusu afya yako kama vile;

  • mizio haswa mzio dhidi ya kiungo chochote katika chanjo
  • mizio yoyote iliyochochewa na chanjo za awali (historia)
  • kama una homa yoyote sasa au uliwahi kuugua hivi karibuni
  • aina zote za madawa unayotumia (kama kunayo), haswa madawa yanayodhoofisha uwezo wa mwili kujiami dhidi ya magonjwa; au dawa za kuzuia damu kushikamana
  • kama u mja mzito (una mimba), unanyonyesha au unanuia kutunga mimba

Kama ilivyo ada na chanjo zingine, usipokee chanjo ya COVID-19 kama una mizio na kiungo chake chochote. Usipokee dosi ya pili kama ulipata mizio kutokana na dosi ya kwanza

Ni muhimu kwa wale ambao tayari wamechanjwa dhithi ya COVID-19, kuendelea kuvaa barakoa, kunawa mikono na kukaa umbali wa mita moja na nusu. Chanzo zinazotumika sasa zinapunguza hatari ya kupata ugonjwa wa COVID-19 kwa takriban asilimia 90 (90%), ikitegemea aina hasa uliyopewa. Walakin, watu waliopokea chanjo ya COVID-19 wanaweza bado kusambaza virusi vya COVID-19 bila kutambua kuwa wanavibeba.

Una weza kupata taarifa zingine muhimu juu ya mada hii katika tovuti hapa:

https://epilepsysociety.org.uk/vaccine

https://www.epilepsy.com/learn/covid-19-and-epilepsy/covid-19-vaccination

https://epilepsysociety.org.uk/news/Covid-vaccine-reassurance

https://livingwellwithepilepsy.com/2020/covid-19/covid-19-vaccine-and-epilepsy.html

 

Last updated: 17 November 2021